Higher Education Students' Loans Board
- Kufanyika Dar Feb 15, 2025
- Rais SMZ kuongoza
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia leo (Ijumaa, Disemba 20, 2024) amezindua mbio za hisani kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa HESLB zitakazofanyika Februari 15, 2025 katika Viwanja vya Farasi (Green Grounds) jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi wa mbio hizo zinazojulikana kama HESLB Marathon, atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Dkt. Kiwia amesema fedha zitakazokusanywa kupitia HESLB Marathon zitatumika kununulia vifaa vya maabara ya shule mbili za sekondari; moja ya Zanzibar na nyingine ya Tanzania Bara. Ameongeza pia kuwa kiasi kingine cha fedha kitatumika kuboresha kituo cha HESLB cha huduma za simu kwa wateja (HESLB Customer Call Centre).